Baada ya CHADEMA, NCCR Mageuzi nao wanena
Baada ya CHADEMA, kuwataka watangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais ndani ya chama hicho wajitokeze, NCCR Mageuzi nao wamesema kuwa wanatarajia kutoa ratiba ya uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Madiwani juma lijalo, na kuiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutenda haki katika uchaguzi ujao.