Balozi Dkt Nchimbi kushiriki mazishi ya Sam Nujoma
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewasili nchini Namibia, akiongoza ujumbe wa CCM kwenye mazishi ya aliyekuwa Rais wa kwanza wa Namibia na Baba wa Taifa hilo, Dkt. Sam Shafiishuna Nujoma, yatakayofanyika Machi Mosi 2025.