Klopp arejea kwenye soka

Jurgen Klopp mwenye umri wa miaka 57 amekubali kurejea kwenye soka lakini kwa kubadili majukumu yake ambapo kocha huyo wa zamani wa vilabu vya Mainz 05,Borrusia Dortmund na Liverpool ataanza kutekeleza majuku yake mapya Januari 1, 2025

Klopp alitangaza kupumzika majukumu yake ya ukocha baada ya kuachana na klabu ya Liverpool mwishoni mwa msimu wa 2023-2024, Kampuni ya Red Bull imefanikiwa kumrudisha kwenye soka baada ya kukubali kufanya kazi ya ushauri wa maendeleo ya michezo kwenye timu zote zinazomilikiwa na red Bull

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS