Kwa ugumu huu nani atakuwa bingwa Italia 2024-25?
Zikiwa zimechezwa raundi 12 za Ligi kuu soka nchini Italia Serie A, mbio za ubingwa zinaonekana kuwa ngumu kwenye michezo hii ya awali ya Ligi. Ambapo timu inayoongoza Ligi ni Napoli wanatofautiana alama mbili tu na Juventus wanaoshika nafasi ya sita kwenye msimamo.