Ijumaa , 24th Apr , 2015

Wasanii wenye uwezo mkubwa katika muziki wa Dancehall kutoka nchini Uganda, Coco Finger na Sheeba wanatarajia kupanda jukwaani kupambana kutafuta nani anamzidi uwezo mwenzake kisanii huko Gulu siku ya kesho.

msanii wa miondoko ya dancehall Uganda Sheeba Karungi

Sheeba na Coco Finger kwa mujibu wa watu wao wa karibu kabisa, wapo fiti huku kila mmoja akiwa tayari kumkabili mwenzake hapo kesho, kila mmoja akiamini kuwa atamkalisha mwenzake.

Mpambano huo unakuwa ni wa kwanza kukutanisha msanii wa kike dhidi ya msanii wa kiume katika jukwaa moja, jambo ambalo linaongeza msisimko na chachu zaidi kwa upande wa muziki huo nchini Uganda.