
msanii wa muziki wa nchini Uganda Desire Luzinda
Staa huyo ambaye anajiandaa kufanya onesho hilo mjini Durban, pamoja na timu ya waratibu bado hawajatoa tamko rasmi, dalili zote zikionesha kutokuwepo kwa onesho, kutokana pia na taarifa za kuwepo kwa machafuko katika maeneo ya pwani ya Durban, watu 5 wakipoteza maisha.
Kwa mujibu wa taarifa, chanzo cha machafuko hayo ni kauli ya mfalme wa jamii ya Zulu, Goodwill Zwelithini kuwa wageni wote nchini humo wanatakiwa kupaki mabegi yao na kuondoka nchini humo.
