Alhamisi , 2nd Apr , 2015

Mahusiano ya mwanadada Zari na Diamond yakiendelea kushika vichwa vya habari, mwanadada huyo amesema kuwa anampenda Diamond, na kuhusiana na mume wake Ivan aliyezaa nae watoto watatu bado wanaendelea kuwasiliana kama kawaida.

Msanii Diamond Platinumz akiwa na mpenzi wake Zari Hassan wa nchini Uganda

Zari ameongea kupitia mahojiano yaliyofanywa hivi karibuni akisema kuwa yeye ni mama wa watoto watatu wa kiume, na amelaumu sana uvumi uliosambaa kuwa ana mtafaruku mkubwa na baba wa watoto wake huyo na hapa anaelezea kama ifuatavyo.

The Boss Lady pia akaamua kuweka hisia zake za wazi kwa staa wa muziki wa Bongo Diamond Platinumz baada ya tetesi zikizidi kuendelea juu ya mahusiano yao ya kimapenzi.