Akizungumza na waandishi wa habari, Museveni alisema kuwa kampuni binafsi mara nyingi huweka mbele maslahi ya faida kuliko huduma kwa wananchi.
Amesema njia sahihi ni Serikali kumiliki na kusimamia njia kuu za kusafirisha data, huku watoa huduma binafsi wakiendelea na biashara zao bila kumiliki miundombinu hiyo ya msingi.
“Kwa namna hii, tutaepuka ukiritimba na kupunguza gharama kwa raia wa kawaida,” amesema Rais Museveni, akiongeza kuwa utandawazi wa kweli unahitaji usawa wa upatikanaji wa taarifa kwa kila mmoja.

