Jumatatu , 24th Nov , 2025

Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba ameagiza kufunguliwa kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima, huku akielekeza lipewe miezi sita ya uangalizi katika kuzingatia miiko, masharti na sheria za uendeshwaji wake.

 Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba ameagiza kufunguliwa kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima, huku akielekeza lipewe miezi sita ya uangalizi katika kuzingatia miiko, masharti na sheria za uendeshwaji wake.

Sambamba na hilo, ameelekeza kurekebishwa kwa sharti linalotaka kufungiwa kwa nyumba ya ibada iwapo atakosea kiongozi, akisisitiza anayekosea ndiye aadhibiwe bila kuathiri waumini kufanya ibada.

“Natambua ilikuwepo hii moja ya Ufufuo na Uzima kaifungulie, ifungulie wape masharti ya uangalizi ndani ya miezi sita. Ziandikie taasisi zote za kidini kuzikumbusha miiko na mipaka ya ufanyaji kazi, sawa sawa na sheria na Katiba ya nchi yetu,” amesema.

Kanisa hilo lilifutriwa usajili, Juni 2, mwaka huu kutoka na kukiuka masharti ya uendeshaji wake, kwa kuhusisha siasa ndani yake.

Dk Mwigulu ametoa kauli hiyo leo, Jumatatu Novemba 24, 2025 alipozungumza wakati wa mkutano wa hadhara, baada ya ziara ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na vurugu za Oktoba 29, 2025.