Paul Pogba
Mara ya mwisho Pogba kucheza mechi ya ushindani ilikuwa Septemba 2023 kwenye mchezo wa Juventus dhidi ya Empoli na anatarajiwa kurejea uwanjani kesho Novemba 22 Monaco itakuwa ugenini kuikabili Rennes.
Nyota huyo wa zamani wa Manchester United alipewa muda wa kuimarisha utimamu wake ambapo awali alitakiwa kuanza mechi yake ya kwanza Novemba 8 dhidi ya Lens lakini ilighairishwa kutokana na kukabiliwa na maumivu ya kifundo cha mguu.
