Jumanne , 21st Oct , 2025

Malkia wa muziki wa Pop Marekani Britney Spears amekiri kupitia kipindi kigumu maishani mwake baada ya kuugua ugonjwa wa Ubongo kwa muda mrefu.

Picha ya msanii Britney Spears

Muimbaji huyo anasema asilimia 100 alipitia changamoto ya uharibifu wa Ubongo jambo lililomfanya kushindwa kuendelea kama msanii japo anashukuru bado anaishi.

Uharibifu wa ubongo unatokea pale seli za ubongo zinapoharibika au kufa na kusababisha matatizo ya kudumu au muda mfupi katika uwezo wa mtu kufikiri, kuzungumza, kutembea, kukumbuka au kudhibiti mwili wake.