
Urusi imeishambulia Ukraine kwa makombora na ndege zisizo na rubani katika shambulio kubwa la usiku kucha, na kuua watu watano na kuharibu miundombinu ya kiraia ikiwa ni pamoja na vifaa vya nishati katika mikoa mingi.
Wanne kati ya waliouawa walikuwa wanafamilia ambao jengo lao la makazi katika eneo la magharibi la Lviv linalopakana na Poland lilipoharibiwa na mashambulizi.
Kwa mujibu wa Meya Andriy Sadovyi, hifadhi ya viwanda katika mji mkuu wa mkoa wa Lviv pia iliteketezwa na sehemu za jiji zikiachwa bila nishati ya umeme, ambaye amewataka wakazi kukaa ndani huku viongozi wakipambana na moto mkubwa katika eneo hilo.
Shambulio la Lviv huenda lilikuwa kubwa zaidi katika vita katika eneo la Lviv, msemaji wa Huduma ya Dharura wa Jimbo hilo amesema kwenye televisheni ya Ukraine.
Katika eneo la kusini-mashariki mwa Ukraine la Zaporizhzhia, mtu mmoja aliuawa na wengine 10 kujeruhiwa katika shambulio ambalo limewaacha zaidi ya watu 73,000 bila umeme, amesema gavana Ivan Fedorov.
Miundombinu ya kiraia pia iliharibiwa katika mikoa ya Ivano-Frankivsk, Vinnytsia, Chernihiv, Kherson, Kharkiv na Odesa, alisema Waziri Mkuu Yulia Svyrydenko.