Jumatano , 25th Jun , 2025

Hizi ndiyo rekodi tano (5) ngumu zaidi kuvunjwa katika michezo.

Nyota wanaoshikilia rekodi katika michezo mbalimbali

1. Cristiano Ronaldo

Nyota wa Timu ya Taifa ya Ureno na Klabu ya Al Nassr Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi ya Kuwa mchezaji mwenye magoli mengi katika michezo ya Kimataifa akiifungia timu yake ya Ureno Magoli 138 timu ya Taifa.

  1. Lionel Messi

Muargentina Lionel Messi anashikilia rekodi ya kipekee ya kufunga magoli 91 ndani ya mwaka 2012 pekee akiwa na timu yake ya Taifa ya Argentina na Klabu ya Barcelona

  1. LeBron James

Nyota wa mchezo wa Kikapu katika Ligi ya NBA ya Nchini Marekani Lebron James anashikilia rekodi ya kuwa Mchezaji aliyefunga alama nyingi katika historia ya Ligi hiyo alifunga alama 42,184 rekodi ambayo hadi sasa bado inaishi.

  1. Usain Bolt

Mwanariadha nguli kutokea Nchini Jamaica Usain Bolt anashikilia rekodi ya kipekee katika mbio za mita 100 akikimbia kwa sekunde 9.58 tu. Rekodi hii aliiweka katika riadha za dunia za 2009 mjini Berlin rekodi ambayo haijavunjwa hadi sasa

  1. Lewis Hamilton

Dereva wa Magari katika mashindano ya Formula One Muingereza Lewis Hamilton akiwa upande wa Ferrari anashikilia rekodi ya dunia ya kuwa dereva aliyeshinda mashindano mengi katika Mbio hizo za magari ambapo hadi sasa ameibuka na ushindi kwa mara 105