Alhamisi , 22nd Mei , 2025

Serikali ya Kenya imekiri kusaidia katika utekaji nyara wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye katika ardhi yake mwaka jana, na kumfanya wakili wake kuishutumu Nairobi kwa kujifanya kama "nchi ya kihuni.

Kizza Besigye, 68, ambaye alifika mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yake ya uhaini siku ya Jumatano, alitekwa nyara na watu wenye silaha katikati mwa mji mkuu wa Kenya mwezi Novemba na kuibuka tena siku chache baadaye katika mahakama ya kijeshi nchini Uganda.

Hapo awali serikali ya Kenya ilikana kuhusika na utekaji nyara wake.

Katika mahojiano ya na wanahabari Jumanne jioni, Katibu wa Masuala ya Kigeni Musalia Mudavadi alikiri kuwa Kenya ilishirikiana na mamlaka ya Uganda katika suala hilo

Akielezea msimamo wake, Mudavadi alisema Uganda ni taifa rafiki na Kizza Besigye hakuwa akitafuta hifadhi na hakusema kama anatafuta hifadhi