Jumamosi , 10th Mei , 2025

Mbunge wa Arusha Mjini amesema kuwa yeye sio Malaika lakini hakuwahi kutumia nafasi yake yoyote ya Uongozi aliyowahi kuitumikia katika kuumiza na kudhalilisha wananchi ama Viongozi wenzakez akiapa kuwa hatomjibu yeyote kwa ubaya na badala yake amemuachia Mungu kwani ndiye ajuaye

Wakati wa mkutano wake wa hadhara leo Mei 10, 2025 kwenye Soko Kuu Jijini Arusha, Gambo amesisitiza pia umuhimu wa kuwahoji wanaomsema, ili waeleze kwa kina mambo yote yaliyotokea, ikiwemo kwa mtu Mmoja ambaye hakumtaja Jina akidai kuwa ni muhimu kwa shutuma anazozielekeza kwake akaeleza pia kuhusu madhaifu yake yaliyomng'oa kwenye nafasi za Umeya Jiji la Arusha na Ukuu wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga.

Gambo amewaambia wananchi wa Arusha kuwa kutokana na kuheshimu familia za watu hao wanaokodishwa kumpakazia Uongo na fitina, ataendelea kuwaombea kwa Mungu ili waweze kupata rizki za kuweza kuhudumia familia zao, akieleza kuwa anafahamu Ugumu wa maisha bila ya kuwa na kazi ama shughuli ya kuingiza kipato kuhudumia familia.