
Uamuzi huo uliotolewa kwa kauli moja unahitimisha miezi kadhaa ya mvutano wa kisiasa ambao umetatiza juhudi za kukabiliana na utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani, wakati huu ambapo taifa hilo la nne kwa ukubwa barani Asia linakabiliwa na kushuka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi.
Waziri Mkuu Han Duck-soo ataendelea kuhudumu kama kaimu rais hadi kiongozi mpya atakapoapishwa ndani ya siku 60 kama inavyotakiwa na katiba.
Mahakama ilikataa hoja nyingi za Yoon ikiziita matumizi mabaya ya wingi wa wabunge, ikisema kulikuwa na njia nyingine za kisheria za kushughulikia mzozo huo.
Lee Jae-myung, kiongozi wa wengi wa chama cha kiliberali ambacho kilishindwa na Rais Yoon kwa tofauti ndogo ya kura kwenye uchaguzi wa mwaka 2022, ndiye mgombeaji mwenye nafasi nzuri ya ushindi lakini anakabiliwa na changamoto za kisheria kuhusiana na kesi nyingi za ufisadi dhidi yake.
Wahafidhina wana uwezekano mkubwa wa kuwasimamisha wagombea.