
Karim Benzema - Mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid
Benzema anashika nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji mabao wa muda wote wa Madrid, nyuma ya kinara Cristiano Ronaldo mwenye magoli 450, huku yeye akiwa amefunga mabao 354 katika kipindi cha miaka 14.
Madrid iliwapa nafasi wachezaji wa zamani katika majukumu mbalimbali ya nje ya uwanja siku za nyuma akiwemo Jorge Valdano na Emilio Butragueno wakiwa sehemu za utendaji. Raul amekuwa akiinoa Real Madrid Castilla tangu 2019, huku Alvaro Arbeloa kwa sasa akiwa kocha wa vijana. Santiago Solari amewahi kuwepo hadi kikosi cha kwanza, huku Zinedine Zidane akijulikana kama mshauri kabla ya misimu miwili ya kuwa kocha mkuu.
Benzema katika mahojiano ya hivi karibuni na Mega alisema kwamba hajui kama ukocha ndio njia anayotaka kuchukua, ila anataka kuwa nafasi kama ya rais Florentino Perez. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 37, kwa sasa yuko katika msimu wake wa pili na wababe wa Ligi ya Saudia Al Ittihad.