
Bondia Abedi Zugo
Kufuatia ushindi huo kumemfanya bondia Soilybaev kuwa bingwa wa Dunia wa mkanda wa UBO katika pambano hilo lililofanyika nchini Kazakhstan katika ukumbi wa Halyk Arena sport complex.
Soilybaev ni bondia namba 27 Duniani kati ya mabondia 1957 kwa uzani wa Super feather akiwa amecheza mapambano 21 akishinda 20 huku 11 kati ya hayo yakiwa kwa 'KO' na akipoteza pambano moja pekee kwa 'points'.
Kwa upande wake Zugo ni bondia namba 67 Duniani kati ya mabondia 1957 akiwa amecheza mapambano 16 akishinda 15 na 13 kati ya hayo akishinda kwa 'KO' na kupoteza moja.