Jumatano , 19th Feb , 2025

Mlinzi wa Arsenal Takehiro Tomiyasu hatocheza tena msimu huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti

Takehiro Tomiyasu - Beki wa Klabu ya Arsenal

Mjapani huyo  mweneye umri wa miaka 26  alijiunga na Arsenal 2021 , msimu uliopita alicheza mechi 30 katika kikosi cha Mikel Arteta wakati msimu huu amecheza dakika 6 pekee dhidi ya Southampton mwezi Oktoba  kutokana na kuandamwa na majeraha

"Nimefanyiwa upasuaji kwenye goti  , imekuwa kipindi kigumu zaidi katika kazi yangu  lakini sitakata tamaa,”  ameandika Tomiyasu

Tomiyasu ataungana na winga wa Klabu ya Manchester United Amad Diallo ambaye pia alipata majeraha katikati yamsimu na kulazimuka kukaa nje hadi mwishoni mwa msimu huu