![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2025/02/07/kijanaa.jpg?itok=4mGhr96s×tamp=1738932692)
Kijana aliyeuawa
Mama wa kijana huyo ameomba vyombo vya sheria kuingilia kati ili haki ya mtoto wake iweze kupatikana kwani waliotekeleza tukio hilo wanawaona mtaani wakitamba kuwa hawawezi kushindana na watu wenye pesa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Machimbo, Evana Isaya amekiri tukio hilo kutokea mtaani kwake, akidai kuwa kijana huyo aliingia kwenye nyumba ya watu usiku hivyo akashambuliwa hadi kufikia umauti wake, huku akiomba wananchi kutojichukulia sheria mkononi kwa matukio hayo.