Serikali ya Sudan Kusini imeondoa marufuku ya muda ya Facebook na TikTok, ambayo iliwekwa wiki iliyopita kufuatia mzunguko wa video zinazoonyesha mauaji ya raia wa Sudan Kusini nchini Sudan.
Picha hizo ambazo zilichochea maandamano, vurugu na mauaji ya kulipiza kisasi kote nchini Sudan, zimeondolewa kwenye mitandao ya kijamii Mamlaka ya Mawasiliano ya Taifa imesema katika barua ya Januari 27 kwa watoa huduma za mawasiliano na intaneti.
"Kuongezeka kwa vurugu zinazohusishwa na maudhui ya mitandao ya kijamii nchini Sudan Kusini kunasisitiza haja ya kuwa na njia ya usawa ambayo inashughulikia sababu za uchochezi mtandaoni wakati wa kulinda haki za watu," Napoleon Adok Gai, mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Taifa, amesema katika barua hiyo.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yalililaumu jeshi la Sudan na washirika wake kwa mashambulizi ya kikabila dhidi ya raia katika jimbo la El Gezira nchini Sudan mapema mwezi huu, baada ya kuuteka mji mkuu wa jimbo hilo Wad Madani.