Takribani watoto 27, wamezaliwa katika Hospitali tatu za rufaa za mkoa wa Dar es Salaam
Takribani watoto 27, wamezaliwa katika Hospitali tatu za rufaa za mkoa wa Dar es Salaam ambapo kwa mwaka huu watoto wakiume ni wengi kuliko watoto wakike ambao ni 10 kati ya 27 waliozaliwa.
Akiongea na EATV, Muunguzi kiongozi wa zamu, Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mwananyamala, Florence Uledi anaelezea watoto waliozaliwa kuanzia saa6 mpaka saa5:59 usiku wa Disemba 25, 2024.
“Tumefanikiwa kuzalisha watoto 10, wakiume nane ambapo mmoja amezaliwa kwa operesheni na wawili wakike wote wapo salama na muda wowote tunaanza kuwaruhusu hakuna mwenye changamoto”, FLORENCE ULEDI-Muunguzi kiongozi wa zamu Mwananyamala Hospital.
Nao baadhi ya wazazi waliojifungua wanaelezea furaha yao kujifungua sikukuu ya Kristman.
“Mimi nina furaha nimejifungu jana mtoto wa kiume anaitwa Noel, nilikuwa natamani nipate mtoto wa kiume na nimefanikiwa kupata mtoto wa kiume kama matamanio yangu”, VERONICA KIHONGOSI-Mzazi.
“Nilikuja saa3 usiku ya tarehe 24, nikajifungua saa6 usiku nimejifungua mtoto wa kike”, MERCY ISSA-Mzazi
Hiyo ilikuwa kwa upande wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mwananyama, lakini upande wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa ya Amana watoto 14 wamezaliwa wakike 7 na wakiume7, kwa upande wa Hospitali ya rufaa ya mkoa ya Temeke wamezaliwa watoto watatu, wakike 1 na wakiume2.