Jumatano , 25th Dec , 2024

Wakati wa ibada ya kusherehekea Krismass mwaka huu Mchungaji wa Kanisa la KKKT Kijitonyama Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dar es Salaam Mchungaji Dkt Eliona Kimaro ameeleza kuwa kupitia Falsafa katika maisha yetu ya Hakuna haki hakuna Amani waumini na vingozi wametakiwa kutenda yaliyomema.

Mch. Dr Eliona Kimaro, Mchungaji Kanisa la KKKT Usharika Wa Kijitonyama Dar es Salaam akihubiri wakati wa ibada ya Krismasi.

Wananchi na viongozi wametakiwa kudumiasha upendo na amani katika kuadhimisha siku kuu ya Krismass ili kuweza kutawala kwa Amani.

Wakati wa ibada ya kusherehekea Krismass mwaka huu Mchungaji wa Kanisa la KKKT Kijitonyama Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dar es Salaam Mchungaji Dakta Eliona Kimaro ameeleza kuwa kupitia Falsafa katika maisha yetu ya Hakuna haki hakuna Amani waumini na vingozi wametakiwa kutenda yaliyomema ili amani iweze kutawala.

"Kabla ya kumaliza leo nitakuwa na Falsafa mbili katika maisha yetu yakwanza ni Jifahamu kwanza ili ufahamike na ya pili ni hakuna haki hakuna Amani amabayo inapatikana katika Zaburi 85:10". Amesema Mch. Dr Eliona Kimaro, Mchungaji Kanisa la KKKT Usharika Wa Kijitonyama Dar es Salaam.

Baadhi ya wachungaji wa makanisa mengine wameongeza kuwa katika siku hii ya leo upendo na matendo mema yanahitajika kudumishwa katika kusherehekea vema siku kuu hii ya Krismasi.
"Katika kusherehekeq siku kuu hii ningependa kuomba waumini wote na watanzania kushiriki na wapendwa wenye uhitaji ili waweze kufurahi kupitia sikukuu hii". Amesema Mch. Kyashama John, Mchungaji Kanisa la John River of Healing.

"Napenda kuwashauri wote kutenda mambo mema na kusherehekea kwa kudumisha amani ili siku ikapate kuwa njema". Amesema Helen Chacha, Nabii Kanisa la Jerusalem Adonai Miracle Chuch- Mwenge Dar es Salaam.

Nae mmoja ya watoa huduma wa nyimbo za injili Japhet Zabron amewataka wananchi kuweza kuitumia siku ya leo vizuri kwa kujikinga na mabaya yote yanayoweza kujitokeza.
"Leo ni siku nzuri kwa kila mmoja kuishi kwa upendo na kuhakikisha upendo unadumu katikati ya kila mmoja anaposherehekea siku kuu hii ya Krismasi". Amesema Japhet Zabron, Mtunzi wa Nyimbo/Mwl. wa Zabron Singers.

"Mimi nawatakia mema wananchi wote kuweza kushiriki vema katika siku kuu hii kwa kutenda mambo mema kwa kila mmoja wetu na kuishi kwa upendo". Amesema Adrian Madale, Mpiga picha Zabron Singers.

Krismasi ni sikukuu ambayo Wakristo wengi ulimwenguni husherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita kila tarehe 25 Disemba.