Yanga SC imeshinda michezo miwili mtawalia ya ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya kwanza tangu ipoteze dhidi ya kikosi cha Tabora United kutokea mkoani Tabora.
Kocha mkuu wa Yanga SC Sead Ramovic amesema maelengo yao ni kuhakikisha wanashinda mchezo wa Ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji, mchezo utakaochezwa kesho Jumatano Disemba 25, 2024. uwanja wa Jamuhuri Dodoma.
Yanga SC imeshinda michezo miwili mtawalia ya ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya kwanza tangu ipoteze dhidi ya kikosi cha Tabora United kutokea mkoani Tabora.
Michezo hiyo kikosi hiko cha mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara pamoja na kombe la shirikisho CRDB kimefunga magoli 8 na kuruhusu magoli 2.
Timu hiyo imebadilika katika ushindi dhidi ya timu za Mashujaa na Tanzania Prisons huku Mshambuliaji alieysajiliwa kutoka kikosi cha Azam Prience Dube akifunga magoli manne katika michezo miwili mtawalia ya ligi kuu Tanzania bara.
Mwenendo huu mzuri wa kimatokeo umekifanya kikosi hiko kufikisha alama 33 kikishika nafasi ya pili nyuma ya Watani wao wa jadi Simba SC inayoongoza ligi ikiwa na alama 34 baada ya kucheza michezo 13 ya ligi.
Wachezaji wa timu hiyo yenye makao yake makuu mitaa ya Twiga na Jangwani wakiendelea kuimarika pamoja na kuizoea falsafa mpya ya Kocha Sead Ramovic raia wa Ujerumani na mrejeo wa Wachezaji waliokuwamajeruhi unaweza kurudisha hamasa ya ushindani pamoja na imani ya kutetea ubingwa wake.
Kesho Disemba 25 Yanga SC itashuka uwanjani kukabiliana na kikosi cha Dodoma Jiji kinachoshika nafasi ya 11 kikiwa na alama 16 baada ya kucheza michezo 14 ya ligi kuu Tanzania bara.