Jumanne , 3rd Dec , 2024

Kocha wa timu ya Simba Fadlu Davies amemzungumzia Mshambuliaji mpya wa timu hiyo Elie Mpanzu kwakuwa anamuumiza kichwa wapi Mchezaji huyo atacheza pale taratibu zote za usajili wake zitakapokamilika.

Klabu ya Simba inashida ya uwepo wa Mchezaji anayeweza kucheza kwa kutokea pembeni ambaye anaweza kufunga na kutengeneza magoli.Viungo wa pembeni wa timu ya Simba wanachangamoto ya kutengeneza nafasi Kibu Denis,Radack Chasambi,Edwin Balua,Joshua Mutale wote mchango wao wa kufunga na kutengeneza nafasi umekuwa mdogo msimu huu.

Kocha wa timu ya Simba Fadlu Davies amemzungumzia Mshambuliaji mpya wa timu hiyo Elie Mpanzu kwakuwa anamuumiza kichwa wapi Mchezaji huyo atacheza pale taratibu zote za usajili wake zitakapokamilika.

Mpanzu Nyota wa zamani wa timu ya AS Vita ya Congo DRC anauwezo wa kucheza namba zote kwenye eneo la ushambuliaji anaweza kucheza winga ya kushoto na kulia, anaweza kucheza namba 9 au Mshambuliaji wa kati pamoja na namba 10.

Klabu ya Simba inashida ya uwepo wa Mchezaji anayeweza kucheza kwa kutokea pembeni ambaye anaweza kufunga na kutengeneza magoli.Viungo wa pembeni wa timu ya Simba wanachangamoto ya kutengeneza nafasi Kibu Denis,Radack Chasambi,Edwin Balua,Joshua Mutale wote mchango wao wa kufunga na kutengeneza nafasi umekuwa mdogo msimu huu.

Endapo Mpanzu ataingia kwenye mfumo wa Mwalimu Fadlu kwa haraka na kufanya kile alichokuwa akikifanya kwenye klabu yake ya AS Vita ya Congo kufunga na kutengeneza nafasi itakuwa faida kubwa kwa klabu hiyo.Uwezo wake wa kucheza Mshambuliaji wa kati utaleta changamoto kwa Steven Mukwala na Leonel Ateba.

Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufunguliwa mwezi huu wa Disemba 15 2024, Mchezaji huyo mpya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi atakapopewa ruksa ya kutumika kwa taarifa zake kuingizwa kwenye mifumo ya TFF na TMS hapo ndipo ataanza kutumika rasmi katika kikosi cha Simba SC.

Winga huyo mwenye kasi na uwezo wa kutumia miguu yote miwili kwa ufasaha anatarajiwa kufanya makubwa kutokana na kiwango chake alichokuwa akikionyesha Congo DR akiwa na AS Vita na timu ya taifa hilo, ongezeko lake linaweza kuleta msaada mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji katika timu ya Wekundu wa Msimbazi akisaidiana na Mukwala na Ateba Mabeki wa timu pinzani wajipange kukutana na Winga hatari mwenye uwezo mkubwa wa kufunga.