Mchezaji huyo kaitumikia timu yake michezo 16 mchezo wake wa mwisho ukiwa Oktoba 6 siku moja kabla ya kupata ajali ya gari akiwa na Rafiki zake.Kaitumikia michezo 3 timu yake ya taifa mchezo wake wa kwanza ukiwa ule wa Novemba 22 dhidi ya Iraq ambao ulitamatika kwa suluhu ya kutokufungana.
Nyota wa timu timu ya taifa ya Ecuador Marco Angulo afariki Dunia akiwa na miaka 22 hospitalini akipatiwa matibabu kutokana na ajaliyopata Oktoba 7 kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo Quito.
Timu yake ya LDU Quito imetoa taarifa kuhusiana na kifo chake kwenye taarifa iliyotolewa leo asubuhi ya Jumanne Novemba 12, 2024 kwenye mitando ya kijamii ya klabu hiyo yenye makao yake makuu Mji mkuu wa nchi ya Ecuador.
Taarifa iliyokuwa ikisomeka '' Kwa huzuni na masikitiko makubwa tunasikitika kutangaza kifo cha Mchezaji wetu Kipenzi Marco Angulo,kilichotokea jana usiku hospitslini alipokuwa anapatiwa matibabu''.
Angulo kabla ya kifo chake hapo jana Jumatatu usiku kafanyiwa operesheni kadhaa na kukaa kwenye chumba cha Wagonjwa mahututi kwa zaidi ya wiki moja.Kahamia timu ya LDU Quito mwezi Machi kwa mkopo wenye kipengele cha kumsajili moja kwa moja akitokea FC Cincinnati inayoshiriki ligi kuu ya nchini Marekani.
Mchezaji huyo kaitumikia timu yake michezo 16 mchezo wake wa mwisho ukiwa Oktoba 6 siku moja kabla ya kupata ajali ya gari akiwa na Rafiki zake.Kaitumikia michezo 3 timu yake ya taifa mchezo wake wa kwanza ukiwa ule wa Novemba 22 dhidi ya Iraq ambao ulitamatika kwa suluhu ya kutokufungana.
Shirikisho la mpira Ecuador limetoa taarifa za kifo cha Mchezaji huyo kwa huzuni na masikitiko makubwa kwakuwa alitizamiwa kuwa Mchezaji atayelitumikia taifa lake kwa muda mrefu kutokana na umri wake.
Taarifa zaidi ya kutokea Ecuador zinasema Mchezaji mwengine wa timu ya Independiente del Valle Roberto Cabezas na Rafiki yake Victor Carcopa,sambamba na Abiria wengine wawili walikuwemo kwenye gari hilo lililopata ajali na hali zao hazijatolewa ufafanuzi wa kina kuhusiana na maendeleo yao.