Jumatano , 30th Oct , 2024

 Fabio Wardley anatizamwa kama Bondia sahihi wa kupanda ulingoni dhidi ya Dubois kutokana na uwezo wake mkubwa ulingoni na rekodi zake. Ameshinda mapambano 17 kwa KO kati ya 18 aliyopigana huku Daniel Dubois akiwa na rekodi ya   KO 21 kati ya mapambano 22 aliyopiyogana.

Bingwa wa masumbwi kwa uzito wa juu ( heavyweight ) anayeshikilia mkanda wa Shirikisho la kimataifa la  ngumi Duniani IBF, Daniel Dubois amepewa muda wa kuamua Mpinzani atakayekutana naye kwenye pambano la kutetea ubingwa wake alioupata mwezi Septemba  baada ya kumshinda  Anthony Joshua.

Pambano la marudiano kati ya Mabondia hao kutoka Uingereza lililopangwa kufanyika mwezi Februari kuna uwezekano wa kutokufanyika kutokana na Promota wa Anthony Joshua Eddie Hearn kuwa na wasiwasi wa Bondia wake kurudi ulingoni kwa haraka baada ya kupoteza pambano dhidi ya Dubois mwezi uliopita.

Rais wa Shirikisho la kimataifa la  ngumi IBF, Bwana Daryl Peoples amethibitisha muda wa miezi 9 aliopewa  Daniel Dubois  ili kumchagua Mpinzani wake atakayekutana naye kwenye pambano lijalo la utetezi wa mkanda wa IBF siku ya Aprili 22, 2025.

Anthony Joshua, kwasasa  hayupo sawa kiakili na kujiamini kwake kumeshuka baada ya kupoteza pambano lake la uzito wa juu dhidi ya Daniel  Dubois mwezi uliopita, ana wiki 10 za kujianda kabla ya kupambana tena mwezi Februari.

 Fabio Wardley anatizamwa kama Bondia sahihi wa kupanda ulingoni dhidi ya Dubois kutokana na uwezo wake mkubwa ulingoni na rekodi zake. Ameshinda mapambano 17 kwa KO kati ya 18 aliyopigana huku Daniel Dubois akiwa na rekodi ya   KO 21 kati ya mapambano 22 aliyopiyogana.

Baada ya tarehe 22 Aprili, IBF itampangia Daniel Dubois pambano lolote ili aweze kupigana kutetea ubingwa wake wa IBF dhidi ya Bondia atakayeibuka mshindi kwenye mpambano wa Martin Bakole dhidi ya Agit Kabayel.

Baada ya tarehe aliyopangiwa kupigana Dubois atakuwa huru kupambana kwenye pambano la kuunganisha mikanda na pambano pekee ambalo linawezekana kutokea litakuwa dhidi ya bingwa kati ya  Oleksandr Usyk vs Tyson Fury ambalo limepangwa kufanyika Desemba 21.

Daniel Dubois anatajwa ndiye Bondia bora atakayetawala ngumi za uzito wa juu kutokea Uingereza kutokana na umri wa Tyson Fury na Anthony Joshua wanaonekana kuchoka kwasasa hivyo Mapromota wa Uingereza wanamtengeneza Dubois aweze kuwa taswira ya mchezo wa masumbwi kwa uzito wa juu Uingereza.