Jumatatu , 28th Oct , 2024

Jeshi la polisi kanda maalumu Dar es Salaam linamshikilia Derick Derick Junior (36) mkazi wa Salasala kinondoni jiji Dar es Salaam kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi sehemu ya jicho na pua Julian Bujuru kwa kumpiga kitako cha bastola.

Taarifa ya jeshi la polisi imeeleza Tukio hilo lililotokea asubuhi ya octoba 27, 2024 katika eneo la masaki 1245 night club, Kinondoni ambapo picha mjongeo zilisambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha tukio hilo na aliejeruhiwa anaendelea vizuri na matibabu.

Aidha jeshi la polisi limeeleza linashirikiana na ofisi ya taifa ya mashtaka kukamilisha utaratibu wa kisheria ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mahakamani.

Sambamba na hilo jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi kuwa halitasita kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote anayemiliki silaha na atakayebainika kufanya matando kinyume na sheria za taratibu za kumiliki silaha.