Bila shaka umewahi kuwaza kuwa ni mara ngapi hasa inakubidi ubadili shuka za kulalia kisha kuzifua? Utafiti wa hivi karibuni wa nchini Uingereza uliohusisha watu takribani 2,250, umeibua mambo mapya kuhusu hali ya ufuaji wa mashuka kwa wanawake na wanaume.
Katika utafiti huo takribani nusu ya wanaume ambao hawajaoa walisema hawafui shuka zao kwa kipindi cha hadi miezi minne hivi , huku 12% wakisema wanazifua wanapokumbuka (inaweza kuwachukua muda mrefu zaidi) .Wakati huohuo, utafiti ulibaini 62% ya wanawake ambao hawajaolewa hufua shuka zao kila baada ya wiki mbili.
Katika kujibu suala hilo Dk Lindsay Browning ambaye ni mwanasaikolojia na mwanasayansi wa neva na mtaalamu wa usingizi wa Uingereza anasema tunapaswa kubadilisha shuka walau mara moja kwa wiki, au hata zaidi na kutofanya hivyo ni hatari zaidi kwa afya.