Safari ya maisha ya wanandoa hawa ilianza tangu mwaka 2007 walipokutana kwenye kongamano la wenye ulemavu wa macho, wanasema licha ya changamoto nyingi walizokutana nazo kwa kipindi chote cha miaka takribani miaka 17 hadi sasa wana watoto watano wanaowategemea.
Wamekuwa kivutio zaidi kwa jamii kwa jinsi wanavyokatiza katika mitaa mbalimbali bila kuhitaji msaada wa watu kuwaongoza, wakisema tayari wameielewa vyema mitaa.
"Yaani siku zote mwanzo ni mgumu, wakati ndio tumeona tulihitaji kuelekezwa kila kitu lakini kwa sasa hata wakati wa kuvuka barabara sisi hatuhitaji kusaidiwa" amesema Bw. Hamis Omary. #EastAfricaTV