Jumanne , 8th Oct , 2024

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imewaachia huru watt watatu waliokuwa wanakabiliwa na staka la kubaka na kumuua binti wa miaka saba aliyekuwa mkazi wa Kimara Temboni jijini Dar es Salaam.

Akiongea Mara baada ya hukumu hiyo mama wa mtoto aliyefanyiwa ukatili Fabiana Gabriel, anasimulia namna mwanae alivyofanyiwa ukatili mpaka kuuawa.

“Nashangaa watuhumiwa wameachiwa huru mwanangu alibakwa na kuuawa haikutosha wakamkata na kitu shingoni, nilikuwa nimemuacha kwa jirani yangu nikaenda kuangalia mabanda Baraka akamchukua mwanangu nimerudi nauliza mwanangu yupo wapi usiku kucha hatujalala kesho asubuhi tunakuta mtoto amebakwa vichakani na kuuawa na kukatwa na kitu chenye ncha kali halafu Leo wanaachiwa huru”, FABIANA GABRIEL-Mama wa marehemu.

 

Nae baba wa marehemu Tumaini Meta,  anasema hawajaridhishwa na hukumu hiyo huku akielezea sababu ya washtakiwa kuachiwa huru.

“Kitu kilichombana ni shahawa iliyokutwa ndani ya marehemu na damu ilipimwa ikakutwa mtuhumiwa namba moja ametenda kosa hilo lakini damu ya marehemu na ya mama yake hazikuandikwa majina kitu kingine jiwe lililotumika kumpiga marehemu kichwani alichukua tarehe 16, na Askari wa pili anasema jiwe lilichukuliwa 17, Sasa wakashindwa kujua hilo la terehe 16 ni lipi na la terehe 17 ni lipi”, TUMAINI

Wakili upande wa watetezi wa washtakiwa Hilda Mushi anaelezea kesi hiyo.

“Hukumu imeweza kutolewa na imebainika kwamba watuhumiwa wote hawana hatia na waneweza kuachiwa huru lakini pia mheshimiwa alienda mbali akasema kwa yeyote ambaye hajaridhika na maamuzi hayo basi walipewa haki ya kukata rufaa”, HILDA MUSHI-Wakili upande wa washtakiwa.