Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deus Sangu
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu katika mahafali ya 37 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kibakwe wilayani humo.
Amesema kitendo cha jumla ya wanafunzi 80 kuacha shule kati ya wanafunzi 247 walioanza kidato cha kwanza mwaka 2021 kutokana na sababu za utoro na mimba, hii inaonesha kuwa kuna baadhi ya wazazi hawawajibiki ipasavyo.
"Leo jumla ya watoto 157 wanahitimu kidato cha nne huku tukiwa tumepoteza watoto 80 kutokana na tatizo la utoro na mimba za utotoni, hii sio sawa wazazi liangalieni hili" amesisitiza Mhe.Sangu
Ameongeza kuwa, "Elimu ndio msingi wa kila kitu ukiamua kuwa mfanyabiashara ni lazima uwe na elimu ukitaka kuwa mjasiriamali ni lazima uwe na elimu ndio maana Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anahakikisha watoto wote wanapata elimu bila ubaguzi wowote" amesisitiza Mhe.Sangu
Kufuatia hatua hiyo Sangu amewataka wazazi kujiepusha na tabia ya kuwaozesha mabinti katika umri mdogo badala yake wahakikishe wanakumbatia elimu itakayowaandaa kwa ajili ya kupambana na maisha
Katika hatua nyingine, Mhe.Sangu amesema Serikali inatarajia kuwapangia vituo vya kazi jumla ya walimu 247 katika Mkoa wa Dodoma hususan katika wilaya ya Mpwapwa kutokana na tatizo kubwa la uhaba wa walimu unaoikumba wilaya hiyo.