Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Freemon Mbowe
Hivi ndivyo Mbowe alivyokamatwa na maafisa wa Polisi na hapa anaelezea kushangazwa kwa nguvu iliyotumika kuwadhibiti waandamani nchini.
"Nguvu kubwa kama hii imetumika kukusanya askari wengi ambao wana silaha nafikiri si sawa sio haki kwa sababu maandamano yetu ni ya amani ni ya maombolezo hayakusudii kumdhuru mtu yeyote, sasa tunasikitika tu nguvu kubwa inatumika kutisha wananchi kunyima uhuru raia", alisema Freemon Mbowe-M/Kiti CHADEMA.
Aidha Mbowe anasema maafisa wa Polisi walikuwa nyumbani kwake toka jana Septemba 2022.
"Nashangaa nguvu iliyotumika kutuzuia, mapolisi toka jana saa3 usiku wapo nyumbani kwangu uzuri sikulala nyumbani nililala hotel", alisema Freemon Mbowe-M/Kiti CHADEMA.
Nao baadhi ya waandamanai waliojitokeza kuandamaana eneo la Ilala Boma wanaelezea kwanini wamejitokeza kufanya maandamano hayo.
"Mimi hata nikiwa peke yangu nitaandamana just imagine mtu anakamatwa kwenye Bus anashushwa mtu mara anakutwa amekufa hapo hatuna imani kabisa", alisema Aurelia Mudiziku-Muandamanaji.
"Mdogo wangu ametoweka karibu mwezi sasa hatujui yupo wapi bora waseme kama amekufa watupe hata mwili tuuzike kuliko hivi hakuna kitu chochjote tunachokijua hatujui hatma za watanzania wenzetu waliotekwa", Eunice Nkya-Muandamanaji.