Jumatatu , 16th Sep , 2024

Waumini wa Dini ya Kiislam mkoa wa Dar es Salaam, wanasema wameadhimisha Sikukuu ya Maulid kwa kuwakumbusha kufanya matendo mema kwenye jamii ambayo wameyarithi kutoka kwa Mtume wao Muhammad (S.A.W).

Msikiti w Mtoro Kariakoo

Leo waumini wa Dini ya Kiislam Tanzania wanaungana  na mataifa mengine Duniani kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad, ambapo husherehekea kwa shangwe , ibada na dua maalum na hujulikana kwa kuleta pamoja waislam wa tamaduni na maeneo tofauti duniani.
Sikukuu ya Maulid an-Nabi hufanyika kila mwaka katika mwezi Rabi’ al-Awwal, ni moja ya miezi mitakatifu katika kalenda ya Kiislam na siku ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), huwa ni sehemu ya sherehe maalum zinazohusisha mijumuiko ys kidini, hotuba na shughuli mbalimbali za kijamii na za kidini.
Na hapa baadhi ya waumi wa Dini hii wanaelezea namna walivyosherehekea sikuu kuu hii muhimu kwenye Dini yao.
“Tunasherehekea kwa kukumbuka matendo mema yaliyotenda na Mtume wetu (S.A.W), kwenye jamii na sisi tunaadhimisha hivyo kwa kutenda matendo mema na kuachana na maovu”, Ashraf Mzee, Muumini wa Dini ya Kiislam.
“Sisi Waislam toka kwenye vita za jadi mpaka inafika hatua kutufanyia usaiji wa hija , tunaadhimisha kuzaliwa kwake kama wenzetu wanavyofanya birthday na sisi mfano wake ndio huu na sisi tunamkumbuka kila kama ibada kwahiyo naadhimisha kwa kuachana na mambo yasiyofaa na yale aliyotuamrisha tuyafate ni kuondoka nayo na hili uweze kuyajua inabidi usome ili uweze kujua mwenyezi Mungu amezungunza nini”, Shabani Awadh, Muumin wa Dini ya Kiislam.
“Tuna furaha kubwa ya kuyapokea na kuyasherehekea mazazi Matukufu ya Mtume na tuliambiwa kuwa Mtume yeye ni Rahma kwahiyo awe Muislam awe sio Muislam anaishi katika Rehma za Bwana Mtume Muhammad kwahivyo tunajivunia na tunafurahikia mazazi yake, kwahiyo tunajivunia mambo mengi ule umoja na ushirikiano wa kiislam tunajifundisha mambo mengi tunakumbuka mambo mengi tunajikumbusha mambo kadha wa kadha ambayo yanatuhusu na yanatupasa sisi umati Muhammad , mengi ya kumfaurahia yale aliyotufundisha utulivu wake, upendo na amani yake, nawakumbusha ndugu zangu waislam kuwa na mshikamano na upendo na udugu na ujamaa maana ndio usislam huo na ndio aliotufundisha Mwenyezi Mungu na akatufundisha Mtume Muhammad (S.A.W), kule kubaguana na chuki ambazo kwamba hazileti manufaa kwetu ni hasara lakini tukiungana kama alivyowaunganisha Mtume wetu Muhammah (S.A.W), akatoka nao kutoka Maka akaenda nao Madina na akajenga Uislam kwa upendo kwa hivyo nasi tubakie na upendo uleule na udugu uleule na ujamaa uleule ndipo tutakapo songa mbele”, Muhamad Noor, Muumini wa Dini Ya Kiislamu.