Maua salum (88), mkazi wa Chanika jijini Dar es Salaam.
Akiongea na EATV, kikongwe huyo anasema baada ya mume wake kupata mke mwingine waligawanywa nyumba hiyo kila mtu vyumba sita lakini cha ajabu akashangaa imeuzwa na kubomolewa bila taarifa yeyote.
"Mume wangu, mtoto wake wa mke mwingine pamoja na mtendaji wa Mtaa, wameshirikiana kunidhurumu namuomba mama Samia anisaidie kupata haki mimi masikini sina msaada wowte na umri wangu huu sina pa kushika popote naomba msaada niweze kupat haki yangu", Maua Salum, Bibi Aliyedhurumiwa.
"Zoezi hili limetekelzwa na mtoto wake mwingine na baba na mtendaji wa mtaa huu wa zamani ambao walituzunguka wakauza mpaka sasa hivi mama hana pa kushi tunaomba Serikali iweze kumpatia msaada wa kisheria", Mohamed Mhina, Mtoto wa mwenye nyumba.
Nae aliyekuwa mpangaji anasimulia tukio la uvunjaji lilivyofanyika.
"Tulistukizia tu kunabomolewa mali zetu zikiwa ndani, tumelifatilia hili swala tukaambiwa twende Mahakamani kila akiitwa hafiki likarudishwa kwa Serikali ya mtaa nako hafiki sasa hili hatujui huyu mama atapata lini haki yake tunaomba Serikali imsaidie" , Humphrey Hauli, Aliyekuwa mpangaji.
Akiongea kwa njia ya Simu mwenyekiti wa mtaa huo, John Ngalawa amekiri kufahamu mgogoro huo huku akielezea namna mauziano yalivyofanyika.
"Mgogoro huo naujua lakini mimi sikuwepo wakati wanauziana na wao waliuziana kwa mwanasheria, baadaye wakapelekana Mahakamni lakini likarudishwa kwa Mkuu wa wilaya kwahiyo lipo juu yangu na mimi sikushuhudia uuzwaji wake na hao wamiliki wanaishi Morogoro kwa sasa hata wakati wanauziana walikuwa wametokea mkoa wa Morogoro", John Ngalawa, M/kiti Mtaa wa Chaurembo.