Akizungumza Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa, amesema tayari kuna vifo vya watoto wawili vilivyotokana na baridi kali na kusisitiza wazazi kuwaangalia watoto wao na kwamba shule ziangalie namna ya kuwa na chai ya tangawizi ili kuwasaidia watoto.
Anthony Mtaka ni Mkuu wa m koa wa Njombe amewataka wazazi waendelee kupewa elimu ya malezi ili watambue nafasi yao katika malezi.
Mkoa wa Njombe kuanzia Mwezi Juni Mpaka Septemba ni kipindi kinachokuwa na hali ya baridi kali jambo ambalo huathiri baadhi ya shughuli za uzalishaji pamoja na ufugaji.