(Bondia Conor McGregor)
Dana White amesema"bado hatujakutana na Conor McGregor lakini tunazungumza na yeye kuhusu urejeo wake ndani ya MMA,anatamani kurejea tena lakini haitokuwa ndani ya mwaka huu zaidi ya tutarajie kurejea tena 2025".
Conor McGregor mwenye umri wa miaka 36 ambaye ni bingwa mara mbili wa UFC alipaswa kupambana na Michael Chandler mnamo Juni 29-2024 kabla ya kupata jeraha la kidole gumba cha mguu huku hajaonekana kwenye ulingo wa UFC tangu avunjike mguu na kupoteze mbele ya Dustin Poirier mnamo Julai 2021.