Jumatatu , 12th Aug , 2024

Jukwaa la Wahariri nchini limevisihi vyombo vya dola mkoani Mbeya, kuwaachia mara moja na bila masharti waandishi watatu waliowakamata jana wakati wakisubiri kufanya mahojiano na viongozi wa CHADEMA waliokuwa wakiendelea na kikao cha ndani kwa sababu kuwapo kwao katika eneo la tukio

Deodatus Balile

walikuwa wanafanya kazi na si sehemu ya siasa au chochote kilichokuwa kinaendelea.

Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Deodatus Balile, na kuwataja waliokamatwa kuwa ni Ramadhan Hamis, Jambo TV, Fadhili Kirundwa, Jambo TV na Francis Simba ambaye ni Mpiga Picha wa Chanzo TV

"Tunalaani matukio ya kukamata waandishi wa habari, matukio haya yanaharibu heshima kubwa ya Tanzania katika kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari aliyoijenga Rais Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021 kwa kurejesha uhusiano mzuri na vyombo vya habari. Sisi Jukwaa la Wahariri Tanzania, tusingependa kuona Tanzania ikirejea katika enzi za giza za kamatakamata. Tunasema waandishi waliokamatwa waachiwe haraka," imeeleza taarifa ya Balile