Makamu Mwenyekiti Taifa wa ACT Wazalendo Isihaka Mchinjita.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti Taifa wa ACT Wazalendo Isihaka Mchinjita,wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Kilwa Kusini ikiwa ni muendelezo wa ziara ya viongozi wa Chama hicho katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Akizungumzia eneo la elimu Mchinjita amesema kwa sasa kuna kundi kubwa la wahitimu wa kada ya elimu wakiwa mitaani ilhali shule nyingi zikiwa na uhaba wa walimu.