Mimba zisizo tarajiwa chanzo cha ongezeko la utoaji mimba usio salama.
Hayo yameelezwa na Afisa Mkunga wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Temeke, Shukrani William, akiongea na EATV kuhusu ongezeko la idadi ya wanawake wanaotoa mimba.
"Mimba hizo zinatolewa kwa sababu hazijapangwa na 45% zinazotelwa kwa njia isiyo salama na kupelekea kupoteza damu nyingi, kutobolewa kizazi au kuondolewa kizazi na kupeleeka wengine kufariki kwa sababu njia ilioyotumika sio salama", alisema William.
Aidha Mkunga anaelezea ni nani naruhusiwa kutoa mimba.
"Cha kwanza sheria hairuhusu mtu kutoa au kutolewa mimba, isipokuwa mwanamke alie hatarini kupoteza uhai wake ndio anashauriwa kutolewa mimba hiyo kwa njia iliyo salama", alisema William.
Je, ni sababu gani zinasababisha mwanamke kutoa mimba?
"Utakuta umepata ujauzito unamwambia mwenzio kuwa uko hivyo anasema yeye haujui anaukataa, na wewe ukiangalia hali yako ya uchumi haupo tayari au upo tu nyumbani mwisho wa siku unaona bora utoe kwani hauwezi kuilea na haujajiandaa kwa malezi peke yako", alisema Lucia Agustino, Mkazi wa Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya vifo vitokanavyo na uzazi ya mwaka 2018 miongoni mwa sababu ya vifo hivyo 10% vimetokana na utoaji mimba usio salama, wananchi wana lipi kuhusu wanawake wanaotoa ujauzito?
"Mimi niwashauri tu vijana kwanza wasome waachane na mapenzi na kama wameamua kuwa na wapenzi na wakapata mimba ni vema wakazaa kwani kufanya hivyo ni makosa au wakishin
dwa basi wattumie njia ya uzazi wa mpango", Janeth Mwekwa, Mkazi wa Dar es Salaam.
"Kwanini wanakuwa tayari kufanya jambo ambalo matokeo yake hawapo nayo tayari, kutoa mimba sio sawa wao wangetolewa wangekuwa wapi, ushauri wangu waachane na kufanya kitu ambacho matokeo yake hawapo nayo tayari", Hassan Mohamedi, Mkazi wa Dar es Salaam.