Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt Moses Kusiluka (kulia)
Balozi Dkt Moses Kusiluka ameitoa kauli leo Agosti 6, 2024, alipotembelea katika maonesho ya kimataifa ya Nanenane katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma na kuipongeza Wizara ya Kilimo pamoja na taasisi zake kwa maandalizi mazuri ya maonesho hayo ambapo amejionea teknolojia mpya za uzalishaji pamoja na tafiti mbalimbali za kilimo.
Balozi Dkt. Kusiluka amefika kwenye maonesho hayo akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe na kuwataka wananchi kwenda kwenye maonesho hayo kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo pamoja na mnyororo mzima wa thamani.