Prof. Shemdoe ameambatana na viongozi na wataalamu wa Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bw. Jabil Shekimweli na kutembelea maeneo mbalimbali yakiwemo vipando vya mahindi, vitunguu, alizeti na mtama.
Maonesho haya yenye hadhi ya Kimataifa yalizinduliwa Agosti 01, 2024 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na kuhudhuriwa na viongozi wa Wizara ya Kilimo; Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Viongozi wa Mikoa, Wilaya, Taasisi mbalimbali Binafsi na za Umma; ikiwa ni pamoja na washiriki kutoka nje ya nchi.