Waziri wa Maji Jumaa Aweso
Amesema hayo leo Julai 23, 2024 akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Morogoro ambapo anakagua mitambo ya kusukuma maji Tumbaku, kukagua shughuli za uzalishaji maji Mafiga, kushuhudia utiaji saini mkataba wa uboreshaji wa huduma ya maji - Gairo na kuongea na wananchi
Amesema Bwawa hilo ambalo ni chanzo kikuu cha maji likitetereka litawaweka wananchi katika mtihani, hivyo ameagiza wahusika kuweka nguvu zaidi katika kulinda na kutunza wa vyanzo vya maji kwa sababu kwenye eneo hilo majani yamesogea mpaka kwenye bwawa.
"Hauwezi ukaruhusu majani yamefika mpaka kule na leo tumekuja tumekuta watu wanakata katakata, jambo la pili tumeona makazi ya watu yanazidi kusogea katika chanzo hiki kikuu cha maji, nafikiri tushirikiane sasa, hii sio kazi ya mtu mmoja, na nyie mkubali pia kushirikisha kwa sababu jamii ipo, na Viongozi wapo usipowashirikisha utakwama tu," amesema Waziri