Freddy Michael Kouablan mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni raia wa Ivory Coast amesema baada ya msimu mbaya zaidi na kutofikiwa kwa malengo ndani ya msimu 2023-24 anaamini timu hiyo itafanya vizuri zaidi msimu baada ya kusajili wachezaji vijana na wenye ubora wa hali ya juu.
“Tupo tayari kwa ajili ya msimu mpya kila mtu anajua jinsi tulivyokuwa na msimu mbaya uliopita na sasa kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya kuipambania timu,rais wa klabu na familia kwa ajili kufanikisha malengo tuliyojiwekea
Kuna wachezaji wengi wapya lakini sio tatizo tunapaswa kuijenga mfumo mpya na timu mpya na wachezaji wapya wanaonesha umahiri mkubwa na kuingia kwenye mfumo tupo hapa kuwapa msaada kutoka kwa manodha mpaka sisi wengine ili kufanikisha malengo yetu tuliyojiwekea”
Nyota Freddy Michael Kouablan alijiunga na Simba SC ndani ya dirisha dogo la msimu 2023-24 akitokea klabu ya Green Eagles ya Zambia huku alifunga magoli 6 ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara huku sasa Simba SC inaendelea na kambi ya maandalizi kwa ajili ya msimu wa mashindano 2024-25 mjini Ismailia nchini Misri