Jumatano , 17th Jul , 2024

Kiungo Mcroatia Luka Modric amesaini kandarasi ya mwaka mmoja ndani ya timu yake ya Real Madrid ya Uhispania utakaomuweka ndani ya miamba ya Santiago Bernabeu mpaka Juni 30-2025.

Kiungo wa Real Madrid Luca Modric

Modric mwenye umri wa miaka 38 ambapo mnamo Septemba 2024 atatimiza miaka 39 amedumu ndani ya Real Madrid Los Blancos kwa misimu 12 na anashikilia rekodi ya mchezaji pekee ndani ya Real Madrid mwenye mataji mengi zaidi kwenye historia ya klabu hiyo.

Luca Modric alijiunga na Real Madrid mnamo 2012 akitokea klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza huku ndani ya Madrid ameshinda jumla ya makombe 26 yakiwemo mataji 6 ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya,Mataji 4 ya La Liga,Mataji 5 ya Spanish Super Cup,na mataji 4 UEFA Super Cup, Nk.