Jumamosi , 13th Jul , 2024

Timu ya Aston Villa ya Uingereza ipo mbioni kukamilisha usajili wa nyota wa Everton FC Kiungo Mbelgiji Amadou Onana kwa ada ya uhamisho wa Pauni Milioni 50 sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 172.1 kwa fedha za Kitanzania.

Kiungo wa Everton Amadou Onana

Onana mwenye umri wa miaka 22 anatakiwa na mkufunzi wa Villa Mhispania Unai Emery kwa ajili ya kuongeza nguvu ndani ya wababe hao wa Villa Park ndani ya msimu 2024-25 ambapo watashiriki kwenye shindano la Ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA)

Amadou Onana ambaye alikuwa anaiwakilisha Ubelgiji kwenye shindano la Euro 2024 nchini Ujerumani na kuondolewa kwenye hatua ya 16 bora na Ufaransa,

Ameitumikia Everton “The Toffees” kwenye  michezo 72 tangu atoke klabu ya Lille ya Ufaransa mnamo mwkaa 2022 huku msimu uliomalizika akiitumikia The Toffees kwenye michezo 37 pekee ndani ya msimu 2023-24