Jumamosi , 13th Jul , 2024

Nyota wa Tenisi Mhispania Carlos Alcaraz amesema anaamini Wahispania watakuwa na siku ya furaha Jumapili Julai 14 ambapo yeye atacheza na Novak Djokovic kwenye fainali ya Grand Slam ya Wimbledon huku timu ya Hispania watacheza na England kwenye fainali ya EURO nchini Ujerumani.

Nyota wa Tenisi Carlos Alcaraz

Alcaraz mwenye umri wa miaka 21 amesema “ Jumapili itakuwa ni siku nzuri kwa Wahispania lakini sitaki kusema kama Hispania itawafunga England  lakini naamini itakuwa ni siku ya furaha sana na kuweza kusherekea mataji mawili siku hiyo”

Rekodi tamu ni 2008 ambapo Mhispania Rafael Nadal alishinda taji la Wimbledon kisha Hispania walishinda shindano la Euro huku mwaka 2010 Rafael Nadal alishinda taji la Wimbledon tena huku Hispania walishinda kombe la Dunia 2010 dhidi ya Uholanzi huku 2023 Nyota Carlos Alcaraz alishinda Wimbledon huku timu ya Wanawake ya Hispania wakishinda kombe la Dunia kwa Wanawake 2023

Fainali ya Wanaume kwenye shindano la Wimbledon inataraji kuanza Saa 11 Jioni nchini Uingereza huku kwa upande wa Fainali baina ya England dhidi ya Uhispania inataraji kuchezwa Saa 4 Usiku mjini Berlin nchini Ujerumani.