Nyota wa Tenisi Jasmine Paolini
Paolini mwenye umri wa miaka 28 anakuwa mwanamke wa kwanza kutoka Italia kufuzu kucheza fainali ya Wimbledon huku atapambana na Mczech Barbora Krejcikova anayeshilia nafasi ya 11 kwenye viwango vya tenisi duniani mnamo Jumamosi ya Julai 12-2024
Fainali ya Wimbledon 2024 inakuwa ni fainali ya pili kwa Jasmine Paolini baada ya kupoteza kwenye mchezo wa fainali ya French Open 2024 mbele ya Mwanadada Iga Switek huku aliishia hatua ya 16 bora kwenye shindano la Australia Open 2024.