Taarifa hiyo imetolewa leo Julai 09, 2024 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, SACP, Issa Suleiman, amesema kuwa mwalimu huyo siku za nyuma alijenga urafiki shuleni na mwanafunzi wa kidato cha nne mwenye umri wa miaka 19 ambaye jina lake limehifadhiwa kwa kuanza kumnunulia vitafunwa shuleni na kumtaka akamtembelee nyumbani, ambapo siku mwanafunzi alipomtembelea nyumbani Mwalimu huyo alianza kwa kumuonesha video chafu kupitia simu yake na baadaye kumtaka amuingilie kinyume na maumbile.
SACP Suleiman ameongeza kuwa, baada ya mwanafunzi huyo kuambiwa hivyo alikataa na kusema hawezi kufanya kitendo hicho ndipo mwalimu akaanza kumtisha kwa kumwambia asipofanya hivyo atapata adhabu kali mara kwa mara shuleni pamoja na kufukuzwa shule na baada ya vitisho mwanafunzi huyo alilazimika kutekeleza kitendo hicho pasipo ridhaa yake.