Jumatano , 5th Jun , 2024

Bei ya mafuta nchini kwa mwezi Juni imeshuka ambapo katika jiji la Dar es Salaam petroli itauzwa kwa shilingi 3,261 kwa lita kutoka tsh 3,314 na dizeli itauzwa kwa 3,112 na mafuta ya taa 3,261.

Mafuta

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imesema mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Juni 2024 yamechangiwa na kupungua kwa bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia (FOB) kwa wastani wa asilimia 11.82 kwa mafuta ya petroli, asilimia 7.77 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 7.94 kwa mafuta ya taa, kuongezeka kwa wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni (Applicable Exchange Rate) kwa 1.4%”

Aidha EWURA wametaja Sababu nyingine ni kupungua kwa gharama za uagizaji wa mafuta (premiums) kwa wastani wa asilimia 2.06 kwa petroli na asilimia 8.51 kwa dizeli katika Bandari ya Dar es Salaam, kuongezeka kwa gharama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 7.07 kwa petroli na asilimia 25.24 kwa dizeli katika Bandari ya Tanga, na zimepungua kwa wastani wa asilimia 12.64 kwa mafuta ya petroli na 12.61 kwa mafuta ya dizeli katika Bandari ya Mtwara.